Ijumaa, 3 Novemba 2017

Mkate wa mayai na zabibu

MKATE WA MAYAI NA ZABIBU

Vipimo

·         Mayai 4

·         Sukari ¼  Kikombe

·         Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula

·         Hiliki ya kusaga ½  kijiko cha chai

·         Baking powder  ½  Kijiko cha chai

·         Zabibu kavu  ¼  kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai  yote manne.


Changanya sukari,  hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.


Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.


Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko  wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.


Mimina unga  ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.


Tupia zabibu  juu ya mchanganyiko wako.


Ingiza sufuria   ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.


Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti  katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.


Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.


Alhamisi, 17 Septemba 2015

VISHETI

Kujua kupika kuna raha yake asikwambie mtu bibie.Na sisi hatuko nyuma kuhakikisha tunakufundsha wewe mapishi mbali mbali na ya uhakika.Tumerejea tena baada ya kuwa kmya kwa mda kdogo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.Tunaendelea na darsa zetu za mapishi kupitia whatsap group zetu kama kawaida.
SIKU:JUMAPILI
MDA:SAA 4:00ASUBUHI
MADA:NAMNA YA KUPIKA VISHETI
KIINGILIO:TSH.2500/=
JINSI YA KUTUMA PESA YA KIINGILIO NI KUPITIA MPESA:0766730322 AU TIGO PESA 0653405342
UKISHATUMA PESA HAKIKISHA UNANIJULISHA KWA KUNITUMIA SMS YENYE JINA LAKO NA NAMBA YAKO YA SIMU ILI NKUUNGANISHE. MWISHO WA KUTUMA KIINGILIO NI KESHO SAA 2 USIKU.

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

KATLESI ZA NYAMA YA KUSAGA

Vinavyohitajika

Nyama  ya  kusaga robo kilo

Chumvi

Mbataa   8 za kiasi

Thomu na tangawizi  iliyosagwa

Pili pili  manga  kijiko  cha  chai

Bizari nzima iliyosagwa  nusu kijiko  cha  chai

Mayai  ya  kuchomea

Mafuta  ya  kupikia

Matayarisho

·         kausha  nyama  yako  na  viungo  vyote.
·         iwache  ipoe.
·         menya  mbatata  zako  uzichemshe   na  uziponde  zikisha  wiva(usisahau kutia chumvi unapozichemsha mbatata)
·         zisubiri   zipoe .
·         tengeneza  mviringo  wa  mbatata  ulizoziponda  na  uweke  nyama  yako  kati. 
·         izibe  nyama  yako kwa mchanganyo  wa  mviringo  wako  wa  mbatata  ulizoziponda.
·         teleka  chuma  chako  cha  mafuta  yawache  yapate  moto.
·         lipige  yai  lako  kwenye  kibakuli tia  chumvi  kidogo.
·         chovya  mviringo  wa  katlesi  yako  kwenye  yai  na  uanze  kuchuma.
·         yai  likiwiva  zitoe   na  uweke  kwenye  chujio  zijichuje   mafuta.
·         ukisha  maliza  weka  kwenye  sahani  tayari  kwa  kuliwa.

Kidokezo

 

Unaweza  kutia  kitunguu maji vidogo vidogo  kwenye   nyama  yako  pia  zina kuwa  nzuri.

Pia kotmiri  kwa  wanaopenda  na  hata  pilipili  pia.

Zikiwa  zinapasuka  unapozichoma  usisahau uzigaragaza  kwenye  unga  wa ngano kidogo  ukisha  ndio  uzichove  yai  na  tayari  kwa  kuchomwa

SHARUBATI YA EMBE

Vinavyohitajika

·         Maziwa  lita 2
·         Kibati  cha mango pulp kimoja au embe fresh iliyomenywa unayoweza kupata pulp.
·         Sukari  kiasi

Namna ya kutayarisha na kutengeneza

·         Mimina maziwa kwenye blender.
·         Pamoja na sukari na mango pulp.
·         Isage kwa pamoja  ichanganyike.
·         Imimine kwenye jagi na uweke barafu ya kutosha.
·         Tayari kwa kunywewa.

Kidokezo

Sharbati hii ni nzuri kwa afya na pia unaweza kuifanya kwa matunda tafauti uyapendayo lakini yasiwe ya ukali tu kwani maziwa yatakatika

BANZI ZA MAZIWA

Vinavyohitajika

Unga  wa  ngano  magi 3

Maziwa  ya   maji  magi  1

Hamira  vijiko  2 vya  kulia

Maji  kiasi

Chumvi kijiko 1  cha  kulia

Mafuta  ya  kupikia  au  siagi  vijiko  2 vya  kulia

Namna  ya  kutayarisha

Changanya  unga, hamira, chumvi pamoja  na  maziwa  vichanganye  pamoja.

Ongezea  maji  kidogo  kidogo  mpaka  uchanganyike  na  uuanze  kuukanda.

Ukande   vizuri  mpaka    ukandike   ulainike.

Chukua   tray  zako  upake  mafuta  na   ukate  madonge  ya  unga  upange  kwenye  tray  uwache  uumke   na  uchome  kwenye  oven  gas  mar  7  au  Jiko    la  umeme  200.

Kidokezo

Hakikisha  madonge   ya  unga yasiwe  makubwa  kama  ya   mikate   ya   kusukuma.

MIKATE YA UFUTA YA KIASILI


Vinavyohitajika

Nazi  kipande  1

Nnga  magi  4

Chumvi

Sukari  kijiko  1  ½  cha  chakula

Ute  wa  yai  1

Hamira  vijiko 3  vya  chakula

Ufuta  wa kutosha

Namna  ya  kutayarisha  na  kupika

·         iroweke  nazi  yako  kwenye  blender  kwa  maji  ya  vuguvugu  na  uisage  vizuri
·         weka  unga  wako   ndani  ya  bakuli  na  utie  hamira, chumvi ,sukari  na  ute  wa  yai
·         changanya  unga  wako  kwa  nazi  uliyokwisha  isaga  (tui)
·         upige  unga  wako   (tofauti  na  kuukanda) namaanisha  unga  huu unazidi  maji
·         ukisha  changanyika  vizuri   unga  wako  ufunike  na  usubiri  uumke
·         ukisha  umka
·         weka  bakuli  la  maji  na utie  chumvi  kiasi(lakini  ukiyaonja  chumvi ijitokeze)
·         weka  chuma  chako  kwenye  jiko  kipate  moto  rushia  maji  yenye  chumvi  kwenye chuma  cha  moto
·         teka  unga  wako  kwa kiganja  cha  mkono  una uutandaze  kwenye  chuma 
·         nyunyiza  ufuta  juu ya  mkate  wako  kabla  haujakauka
·         utie kwenye   grill  hapo  utaumuka  na  kuwiva  kuwa  rangi  nzuri  ya  kuvutia
·         rejesha  tena  juu  ya  jiko  kwa moto  wa kiasi  na  uupake  mafuta  kwa  brash 
·         utoe  na  uuweke  sahanini  tayari  kwa  kuliwa.

Kidokezo

Ukitia  yai  na kiini  chake  cha  manjano  utachelewa  kuumka  na  hautakuwa  na  rangi nzuri  ya   kuvutia